Thursday, August 21, 2008
WANANCHI WA AFRIKA TUCHUKUE HATUA
Hakika unapochukua muda kutafakari hali halisi ya afrika unaweza kujikuta unamwaga machozi.Kama kubarikiwa na Mungu basi Africa imebarikiwa,kila kitu cha asili kipo afrika. lakini hali ya watu wa Afrika inatisha.Lakini shida hii itatatuliwa na waafrika wenyewe.Hebu jaribu kufikiri nchi kama Tanzania yenye madini ya ulanga,dhahabu,almasi,chuma pamoja gesi,maziwa makubwa,mito mikubwa,misitu,ardhi yenye rutuba na vitu vya asili vingi ambavyo Mungu ametubariki navyo lakini hali halisi ya watanzania wenyewe ni choka mbaya.Tunachohitaji ni viongozi imara wenye msimamo na uzalendo wa kweli wa nchi hii kwani nchi za afrika wenye kuzifaidi ni hao maarufu kama "MAFISADI" watu wasio na uchungu na nchi wala raia.Ushauri mkubwa uliopo ni kuwa wenye uwezo wa kuiponya afrika ni waafrika wenyewe.Tuachwe kudanganywa na viongozi wenye kufanya mambo mazuri wakati uchaguzi unakaribia au kuhonga ili apate kula kwani wakishapata kula hela yao na gharama zote walizozitumia lazima wazirudishe na ndio hapo ule msingi wa kurudisha pamoja na roho ya kinyama waliyonayo inapelekea hali za mamilioni ya watu kuwa mbaya zenye kukatisha tamaa hali wakicheka na kufurahi.Ndugu zangu watanzania uchaguzi wa 2010 tusicheke na viongozi wabovu eti kwa sababu ni wajomba au mabibi au jitihada walizozionyesha mwishoni.Walitakiwa waanze mwanzoni. Usijitie unasikitikia hali za watu wakati wewe mwananchi ndio wa kwanza kuwashabikia viongozi ambao unajua kabisa wataangamiza wananchi na uchumi kw ujumla huo ni unafiki mkubwa.Masikitiko na uchungu wa kweli wa kuleta mabadiliko Afrika unaweza kuonyeshwa pale tu tunakapochukua hatua ya kukataa dhuluma hizi hasa zinazofanywa na viongozi kwa kutokubaliana nao na kuonyesha msimamo wa dhati.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comment:
A good stuff,best wishes in the coming elections,play it well,play it properly,stay smart till day zero.
Post a Comment